Skip to content
Wellness

ambacho hujakijua bado kuhusu insulin

HealthTalks makala ya afya na tiba.

EL
elibarikiisrael27
Mar 2, 2026·Dakika 4 kusoma
ambacho hujakijua bado kuhusu insulin

Ambacho hukukijua kuhusu Insulin

Watu wengi wanaifahamu insulin kwamba inafanya kazi ya kuthibiti viwango vya sukari katika damu ila kuna mengi ya kujua zaidi

Insulin ni moja kati ya protini ndogo zaidi mwilini ,sio tu protini ni protini special ndio maana ni miongoni mwa homoni ,japo ni ndogo sana kazi yake ni kubwa mno mwilini mwako

Waza hivi seli za mwili wako ni kama nyumba na ili ziweze kuishi zinahitaji nishati (hasa glucose ) ambayo unaipata kwenye chakula ulichokula ila sasa glucose hiyo haiwezi kuingia ndani ya seli kirahisi tu inahitaji ufunguo na insulin sasa

Ndio ufunguo wenyewe hapa unapokula kongosho huzalisha insulin na Insulin husafiri hadi kwenye seli na kuzifungua na kuruhusu sukari iingie ili iweze kutumika kama nishati insulin pia inafanya kazi zingine nyingi kama

  1. Kwanza ni homoni ya anabolic namaanisha kwamba inasaidia kujenga vitu mwilini
  2. Uhifadhi wa Nishati hapa kwa mfano una sukari nyingi kwenye damu insulin hutoa taarifa ili ini na misuli yako kuhifadhi sukari hiyo kama glycogen kwa matumizi ya baadaye ndio maana unaweza bado ukawa na nguvu hata usipokula kwa muda mrefu kidog
  3. Uzalishaji wa Mafuta: sasa akiba ya glycogen inapojaa insulin hutoa ishara kwa mwili kubadilisha ile sukari ya ziada kuwa mafuta kwa ajili ya akiba ya muda mrefu
  4. Uzalishwaji wa protini: Ndio maana ni muhimu kwa ukuaji wa misuli baada ya kufanya mazoezi

Uwiano wa Madini: Inasaidia hasa kudhibit kiasi cha madini ya potasiamu yanayoingia kwenye seli na kufanya moyo wako muda huu udunde kwa kawaida

Bila homoni hii ndogo seli zako zingekufa kwa njaa hata kama sukari ingekuwepo kwenye damu

Natumaini umeelewa
Ungependa kujua kuhusu nini zaidi?

#Raisinghealthygenerations

Was this post helpful?

Related articles

Endelea kujifunza kuhusu afya na uzima kupitia makala zetu za kitaalamu.

View All →