Ruka hadi kwenye maudhui
Disease Prevention

Je, Unajua? Baadhi ya Saratani Husababishwa na Virusi?

HealthTalks makala ya afya na tiba.

EL
elibarikiisrael27
17 Feb 2026·Dakika 4 kusoma
Je, Unajua? Baadhi ya Saratani Husababishwa na Virusi?

Ni sahihi kabisa aina kadhaa za saratani huchochewa na maambukizi ya virusi

Jinsi Inavyotokea?

Saratani inatokea pale seli zinapogawanyika tu bila mpangilio sasa baadhi ya virusi huvuruga mpangilio wa mgawanyo wa seli kwa kufanya moja kati ya haya

  1. Baadhi ya virusi hubeba vinasaba (genes) ambazo zinapoingia kwenye DNA katika seli za mtu hulazimisha seli kugawanyika bila mpangilio kitaalamu inaitwa “Oncogenesis”
  2. ⁠Pia kikawaida katika seli vipo vinasaba (genes) ambazo kazi yake ni kuzuia saratani sasa vinasaba hivi vikiharibiwa na virusi matokeo yake ni kwamba saratani hutokea kirahisi zaidi

Mifano ya Virusi vinavyosababisha saratani
Saratani ya Mlango wa kizazi karibu asilimia 90 husababishwa na kirusi cha HPV (yaani Human Papillomavirus) , pia saratani ya Ini mara nyingi huchochewa na virusi vya Hepatitis B au C

Unachopaswa kukijua leo
Ni kwamba saratani zinazotokana na virusi ni miongoni mwa saratani zinazozuilika kwa urahisi zaidi kwa njia hizi hapa

  1. Chanjo ,saratani zilizotajwa hapo juu hukomeshwa kwa ufanisi sana kwa chanjo hivyo hakikisha unapata chanjo
  2. ⁠Uchunguzi wa mapema husaidia kugundulika mapema na kupata matibabu sahihi

Usisahau kushare ujumbe huu na unaowajali

Ungependa kujua kipi zaidi?
#Taarifa sahihi maamuzi sahihi #war on cancers

Je, makala hii imekusaidia?

Makala Zingine Zinazohusiana

Endelea kujifunza kuhusu afya na uzima kupitia makala zetu za kitaalamu.

Tazama Zote →