Ruka hadi kwenye maudhui
Wellness

sayansi ya kinga ya mwili

HealthTalks makala ya afya na tiba.

EL
elibarikiisrael27
13 Feb 2026·Dakika 4 kusoma
sayansi ya kinga ya mwili

Unaposoma ujumbe huu kuna uwezekano mkubwa kuwa mfumo wako wa kinga unashughulika moja kati ya haya

  1. Kupambana na maambukizi (kama yapo)
  2. Kuondoa seli zilizoharibika,kuponya jeraha
  3. Au hata kuzuia saratani

Unaeza hata usijue kwamba hiki kinaendelea labda upo bize na mambo yako ila kinga yako ya mwili ipo kazini

Huu mfumo ni muhimu sana kwa ajili ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa, maambukizi na uharibifu

Ni ngumu sana kufikiria maisha bila mfumo huu ndio maana utaukuta kwa kila kiumbe kuanzia wewe hapo ,mimea ,wadudu ,hadi bacteria ambaye ni seli moja tu naye ana mfumo wa kinga kwajili ya ulinzi

Mfumo wa kinga una nguvu sana lakini pia una nidhamu ,nidhamu ambayo inauzuia usikudhuru wewe mwenyewe

Ila sasa muda mwingine nidhamu hiyo hupotea na mfumo uleule wa kinga ambao ulitakiwa kukulinda hugeuka na kuanza kukushambulia na kuleta madhara mwilini

Hii hali inajulikana kama Auto-immune diseases mfano magonjwa kama kisukari aina ya kwanza ,Multiple sclerosis, lupus na mengine

Natumaini umejifunza kitu , ungependa kujua nini kuhusu kinga ya mwili?

Je, makala hii imekusaidia?

Makala Zingine Zinazohusiana

Endelea kujifunza kuhusu afya na uzima kupitia makala zetu za kitaalamu.

Tazama Zote →